BY AMRIY RAJABU DIMOSO
Hali katika kampuni ya RJ inayoongozwa kwa ubiya kati
ya Vicent Kigosi ( Ray) na Blandina Chagula ‘Johari’, inazidi kuwa tete
kwa kile kinachoelezwa kuwa johari hataki kufanya kazi pamoja na ‘mke
mwenza’ Chuchu Hans.
Chanzo hicho ambacho kipo karibu na wasanii hao kilisema kuwa mwezi
mmoja uliopita Johari na Chuchu, walikuwa katika kuelekea kuelewana
ambapo johari, alishakubali yaishe kuwa Ray wake ameshapokonywa na mtoto
huyo wa Kitanga .
Mnyetishaji huyo aliendelea kusema kuwa baada ya Johari kuwa katika hali
hiyo,ndipo Chuchu alipoanza kutanua makucha yake ndani ya kampuni kwa
kujifanya ni mmoja kati ya wakurugenzi wakati ukweli haupo hivyo.
Chanzo hicho kilizidi kusema kuwa imefikia hatua Chuchu, kaanza kutoa
amri kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo bila ya kupata kibali kutoka kwa
wakurugenzi waasisi ambao mtaji wao unadaiwa kutokana na Johari
‘kumpiga’ changa la macho mfanyabiashara maarufu kutoka mkoani Mbeya.
Mpashaji huyo alizidi kusema kuwa bifu liliibuka upya mkoani Dodoma,
ambako Ray na Johari walikwenda katika ziara ya Kilimanjaro Music Awards
Tour, na mashabiki wao kuwataka wapande jukwaani kwa pamoja.
Mtoa habari hiyo alisema kuwa
kuwa kutokana na hali hiyo, ndipo Chuchu alipoanzisha bifu la chinichini
lililopelekea hadi sasa kwenye kampuni hiyo kuzuka mtafaruku mkubwa
huku Johari, akitaka kujitenga kabisa na Ray lakini kinachomkwamisha ni
pesa zake nyingi alizowekeza.
Inadaiwa kuwa Johari amekuwa mkali sana sasa hivi akimtaka mkurugenzi
mwenzake Ray, wagawane kila kitu mpaka nguo za ndani walizonunua kwa
pesa za kampuni yao hiyo.
Katika kufuatilia habari hizo ili kupata ukweli kuhusiana na timbwili
hili mwanahabari wetu aliwasaka wote kwenye simu zao za mkononi, lakini
wote hawakutaka kutoa ushirikiano kwa kile walichokieleza kuwa wapo bize
na maswala binafsi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni