Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh. Nape Nnauye, Jumatatu hii, March 20, alikwenda katika makao makuu ya Clouds Media Group kufuatia taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenda kwenye kituo hicho akiwa na askari wenye silaha na kuwataka watangazaji wa kipindi cha Da W’keend Chat Show kurusha kile alichokiita kipindi chake.
Waziri Nape ameunda tume ya uchunguzi ya watu watano watakaongozwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo, Hassan Abbas, na kutoa masaa 24 kwa tume hiyo kuzungumza na Mkuu wa Mkoa Makonda na kutoa ripoti yake Jumanne hii, March 21, 2017.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni