Utangulizi
Tuzo za watu Tanzania ni tuzo za aina yake, zilizoanzishwa kwa mara ya kwanza nchini mwaka 2014, mahsusi kwaajili ya kuwapa mashabiki wa muziki, filamu, michezo na burudani, jukwaa huru kuwapendekeza na hatimaye kuwachagua washindi wanaowapenda na kuwakubali katika vipengele vilivyoainishwa kwenye Tuzo Za watu 2014.
Tuzo hizi zilitambulishwa na kuratibiwa kwa mara ya kwanza Tanzania mnamo Aprili mwaka 2014 na kuhitimishwa mwezi Juni mwaka huo, na kutarajiwa kuendeshwa kila mwaka.
Upekee wa tuzo hizi ulikua ni kwamba majina yote ya washiriki walioshindanishwa kuwania tuzo, kuanzia mwanzo wa mchakato mzima hadi mwisho yalichaguliwa na wananchi wenyewe na sio kundi la watu wachache (kamati) kwenye tasnia husika, kama jinsi ambavyo imezoeleka . Wananchi wenyewe walipendekeza washiriki na hatimaye kuwachagua washindi na hivyo kuzitofautisha tuzo hizi na tuzo zingine nchini.
Tuzo za watu zinadhamiria kuendelea kuhamasisha mchakato wa wazi na huru wa utambuzi wa watu wenye umuhimu na michango mahsusi katika nyanja mbalimbali, ambao wanachaguliwa moja kwa moja na wananchi wenyewe. Kutambulika huku kutachangia kuikuza tasnia ya sanaa nchini pamoja na kuinua vipaji vya wasanii na vile vile kuhamisha kuibuka kwa vipaji vya kutoka kwenye jamii.
Washiriki wote waliosalia baada ya kufanyika mchujo wa mwisho, watakuwa wageni wa heshima kwenye utoaji wa tuzo hizo. Katika hafla hiyo, washindi watatangazwa na kila mshindi atapokea zawadi ya fedha taslimu, shilingi 1,000,000 za Kitanzania pamoja na tuzo.
Mifumo wa Upigaji Kura
Mchakato wa kupendekeza majina ya washiriki katika tuzo hizi utafanyika kwa njia kuu mbili.
Kwanza ni kwa kupitia tovuti ya tuzo hizi ambayo ni www.tuzozetu.com
Kwenye tovuti hii, mpigaji kura atakutana na hatua rahisi ya kupendekeza majina katika vipengele vyote vya tuzo za watu Tanzania.
Njia ya pili itakua kupitia simu ya mkononi kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno, ambapo mpigaji kura atahitajika kuandika neno ‘TUZO’ na kutuma kwenda namba 15678.
Baada ya kutuma ujumbe huu, ataletewa vipengele vyote vikiambatanishwa na TZW kifupi cha Tuzo Za Watu, pamoja na namba ya kila kipengele. Ili kutaja ama kupendekeza jina, atahitjika kutuma ‘code’ husika na jina kwenye namba hiyo hiyo; kwa mfano TZW1 Michael Jackson.
Ratiba
14 April – Mwisho upigaji kura awamu ya kwanza.
16 April – Orodha ya majina matano ya waliyoongoza kwa kura zaidi, kwenye kila kipengele kati ya vipengele 14 zitatangazwa, mwanzo wa upigaji kura awamu ya pili.
16 April – Orodha ya majina matano ya waliyoongoza kwa kura zaidi, kwenye kila kipengele kati ya vipengele 14 zitatangazwa, mwanzo wa upigaji kura awamu ya pili.
23 April – Mwisho wa upigaji kura awamu ya pili.
24 April – Orodha ya majina manne ya waliyoongoza kwa kura zaidi, kwenye kila kipengele kati ya vipengele 14 zitatangazwa, mwanzo wa upigaji kura awamu ya tatu.
24 April – Orodha ya majina manne ya waliyoongoza kwa kura zaidi, kwenye kila kipengele kati ya vipengele 14 zitatangazwa, mwanzo wa upigaji kura awamu ya tatu.
30 April – Mwisho wa upigaji kura awamu ya tatu.
01 May – Orodha ya majina matatu ya waliyoongoza kwa kura zaidi, kwenye kila kipengele kati ya vipengele 14 zitatangazwa, mwanzo wa upigaji kura awamu ya nne na ya mwisho.
01 May – Orodha ya majina matatu ya waliyoongoza kwa kura zaidi, kwenye kila kipengele kati ya vipengele 14 zitatangazwa, mwanzo wa upigaji kura awamu ya nne na ya mwisho.
14 May - Mwisho wa upigaji kura.
16 May – Hafla ya kuwatangaza washindi na utoaji tuzo.
16 May – Hafla ya kuwatangaza washindi na utoaji tuzo.
Washiriki wote watakaofika fainali ya kuwania tuzo (watatu katika kila kipengele) watakuwa wageni wa heshima kwenye utoaji wa tuzo hizo.