LOH!! KUMBE DIAMOND KAWADANGANYA WATANZANIA KUHUSU KUSHINDA TUZO MBILI
WASANII wa Tanzania wenye mashabiki wengi Afrika Mashariki, Lady Jay Dee na Diamond Platinumz, wameitoa Tanzania Kimasomaso kwa kushinda tuzo moja moja katika tuzo za AFRIMA (African Muzik Magazine Awards 2014), zilizofanyika jana Dallas, Marekani.
Kwa mujibu wa mtandao wa African Music Magazine, Lady Jay Dee alishinda tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa Afrika Mashariki na Diamond Platinumz alishinda tuzo ya Msanii bora wa kiume wa Afrika Mashariki.
>>MWANAUME AMBAYE YUKO "PERIOD"( HEDHI) AGUNDULIWA, WAMKUTA NA MAYAI YA UZAZI YA KIKE::CHEKI HAPA
Hata hivyo, kwa habari ambazo zimeenea Tanzania na kutajwa kuwa zilizotolewa na meneja wa Diamond zinaeleza kuwa Diamond ameshinda tuzo mbili ambayo nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana.
Hali hiyo ilisababisha utata, kwa mashabiki wa mwanamuziki huyo Diamond Platnamu hali iliyopelekea mashabiki hao kuhisi kuwa msanii huyo amewadanganya mashabiki wake.
>>>KICHANGA CHAKUTWA HAI KATIKA TUMBO LA MAMA ALIYEUAWA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni