WALIOTENGENEZA PICHA MBAYA KUMHUSU MAMA YAKE WEMA SASA KUKIONA CHA MOTO, WEMA NA MAMA YAKE WAPANGA HAYA....
SIKU chache
zimekatika tangu kusambazwa kwa picha feki inayodaiwa ni ya mama wa
Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu, wawili hao wako kwenye
mkakati mzito wa kuwasomea kisomo cha Albadili wale wote waliohusika kwa
namna yoyote ile kuitengeneza picha hiyo na kuitupia mitandaoni, Risasi
Jumamosi linakumegea.
Picha
hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa na
kichwa cha mama Wema, lakini sehemu ya kuanzia shingoni kwenda chini si
yeye na mhusika alikuwa hana nguo, ilizua gumzo kwa wiki mbili sasa huku
watu wanaojiita Timu Dengue wakitajwa kuhusika.KINYWANI MWA CHANZO CHA HABARI
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mama Wema na mwanaye wameamua kusoma Albadili ili kuwaadabisha wale wote waliohusika na sakata hilo lenye kufedhehesha.
“Mama Wema na mwanaye walikasirishwa sana na watu waliotengeneza ile picha na kuitupia kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram.
“Wiki iliyopita baadhi ya wasamaria wema walikwenda nyumbani kwa mama Wema na kumtajia majina ya wahusika, lakini hawakuwa na ushahidi hivyo yeye na Wema wameamua kujiunga kiimani zaidi kwa kusoma Albadili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni