Takriban watu 150 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab, katika eneo la Garisa, nchini Kenya. Katika tukio hilo la kinyama lililotokea saa 11 asubuhi kwenye Chuo Kikuu cha Garisa, magaidi hao waliwapiga risasi na kuwachinja wanafunzi Wakristo.baada ya kuwazidi nguvu walinzi.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la hapa Uingereza, idadi ya waliouawa inafikia 147 na majeruhi ni 79 huku watu 500 wakiokolewa. Wengi wa waliouawa na wanafunzi wa chuo hicho, pamoja na polisi wawili,mwanajeshi mmoja na walinzi wawili.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Joseph Nkaissery , alieleza kuwa magaidi wanne walijifunga mabomu, na polisi walipowapiga risasi, walilipuka kama mabomu ambapo vipande vya mabomu hayo viliwahjeruhi polisi.

Maafisa wa usalama katika eneo la tukio walieleza kwamba mateka kadhaa waliokolewa, na magaidi wanne waliokuwa na bunduki aina ya AK-47 waliuawa.

Jana usiku, Kituo cha Operesheni ya Uokoaji Kitaifa kilieleza kwamba idadi ya wanafunzi wote, wazima na waliouawa sasa inafahamika.

Shambulizi hilo linaelezwa kuwa baya zaidi nchini humo katika miaka 17 baada ya shambulizi jingine kubwa la kigaidi mwaka 1998 kwenye Ubalozi wa Marekani nchini humo ambalo lilipelekea vifo zaidi ya 200.

Tukio hilo la jana limetokea katika Juma Kuu, kipindi cha majonzi katika kalenda ya Wakristo. Jana ilikuwa Alhamisi Kuu ambayo kwa mujibu wa taratibu za baadhi ya madhehebu ya Kikristo, ni siku ya maungamo. Leo, Ijumaa Kuu, ni siku ya maadhimisho ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo msalabani na hatimaye kufa. Jumapili ijayo ni Pasaka ambapo Wakaristo wanaadhimisha ufufuo wa Yesu Kristo.

Maafisa usalama wa Kenya walieleza kuwa gaidi mmoja alikamatwa wakati anajaribu kutoroka. Kadhalika, serikali ya nchi hiyo imetangaza zawadi ya Shilingi za Kenya Milioni 20 kwa atakayewezesha kukamatwa kwa Mohammed Mohamud, anayejulikana pia kama Dulyadin, au Gamadhere, ambaye anatuhumiwa kupanga shambulizi hilo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni