Alhamisi, 17 Julai 2014

LULU ATIA FORA

 

Mchecheto! Staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, hivi karibuni alijikuta akiendelea kuwehukia penzi la mwanamuziki Mkanada anayefanya shughuli zake nchini Marekani, Justin Drew Bieber (20), Amani  lina cha kushika mkononi.Staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’,
Ishu hiyo ilitokea Julai 14, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa BoT uliopo maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam ambapo wasanii wa Marekani waliotinga Bongo kwa mwiliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ walikuwa wakitoa semina kwa wasanii wa Bongo.
Lulu ambaye kwa miaka mingi amekuwa akiweka wazi mapenzi yake kwa Bieber alifika ndani ya ukumbi huo na kumwambia staa mwenzake wa sinema, Zuweza Mohamed ‘Shilole’ kwamba lengo la kufika kwake ni kuwaomba wasanii hao namba za simu za Bieber.
ILIKUWAJE?
Semina hiyo ilikuwa na lengo la kutoa mbinu za namna ya kukuza na kupanua soko la muziki na sanaa zote Tanzania.
Semina ilianza saa 3:00 asubuhi na wasanii wa Bongo waliitikia wito kwa kufika mapema, lakini Lulu alizama ukumbini hapo saa 8:12 mchana.