Jumapili, 1 Novemba 2015
Jumatatu, 1 Juni 2015
Mwigulu na Wassira wakoleza mbio za Urais
Mwigulu na Wassira wakoleza mbio za Urais
MAKADA wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba na Stephen Wassira wametangaza rasmi nia yao ya kutaka kuwania kupitishwa na chama hicho, kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwigulu ambaye ni mbunge wa Iramba Mashariki, alitangaza uamuzi wake huo mjini Dodoma wakati Wassira alitangaza nia hiyo jana jijini Mwanza mbele ya viongozi, wanachama na waasisi wa TANU na CCM na wananchi.
Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa chuo cha Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kauli ya Wassira Akihutubia mamia ya wakazi waliofurika katika maeneo ya chuo hicho, alisema ameamua kutangaza nia yake hiyo kwa sababu anao uwezo mkubwa wa ndani na nje wa kuongoza nchi.
Pia, alisema amefanya hivyo ili kuvunja baadhi ya minong’ono kutoka kwa baadhi ya watu, iliyomtaka kutangaza nia hiyo. Aliainisha mambo makubwa matano, ambayo atayatekeleza endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.
“Niwashukuru sana kwa kuacha kazi zenu na mkaja hapa kushuhudia jambo hili muhimu, kwa zaidi ya mwaka mzima kumekuwepo na minong’ono kutoka kwa juu ya mimi kuwania urais, leo nimekuja hapa Mwanza kuvunja minong’ono hiyo na kutangaza wazi kuwa natangaza rasmi kuwania nafasi hiyo”, alisema.
Alisema ameamua kujitokeza kuwania nafasi ya urais, kwa kuwa yeye ni mtu sahihi kuongoza nchi. Alisema amefanya kazi kwa karibu na marais wote wa nchi hii, waliopita tangu awamu ya kwanza hadi ya sasa na kwamba alikuwa na fursa pekee ya kuwasiliana nao.
Aliongeza kuwa sababu nyingine iliyomsukuma kuwania nafasi hiyo ni kuwa anaijua vizuri Tanzania kwa kuwa ameshiriki katika siasa za nchi akiwa angali kijana mdogo wa umri wa miaka 25.
“Mwaka 1970 nikiwa na umri wa miaka 25 nilichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo langu la Mwibara wilayani Bunda na nimewatumikia watanzania katika nyadhifa nyingi za juu kwa miaka 45 iliyopita kwanza kama Mbunge, Mkuu wa mkoa, Naibu Waziri na baadaye Waziri kamili katika awamu mbalimbali”, alisema, na kuongeza,
“Baada ya tafakari ya muda mrefu na ya kina kwamba nimeamua ni sahihi, ni wakati mwafaka na kwa hakika, mimi ndiye mtu sahihi wa kujitokeza na kuwahudumia watu wa nchi hii “, alisema.
Vipaumbele vyake
Alitaja baadhi ya vipaumbele anavyotarajia kuvitekeleza katika Serikali yake, endapo watanzania watamchagua kuwa Rais kuwa ni kuteng’eneza nafasi za ajira kwa vijana, kujenga uwezo wa watanzania kushiriki kikamilifu katika ukuzaji wa uchumi, kuwekeza katika watu, ikiwa ni pamoja na kufumua upya mfumo wa elimu ili kuwezesha wafanyakazi kuwa na ushindani.
Wasira alivitaja vipaumbele vingine atakavyovitekeleza kuwa ni pamoja na kuwa na ujenzi wa miundombinu inayoendana na mazingira ya Karne 21, yenye dhamira ya kukuza uchumi wa nchi, kuwezesha ushiriki mpana wa demokrasia na maendeleo ya kiuchumi sanjari na utekelezaji wa mipango, Sera na mikakati mbalimbali ya kiserikali.
“Nitaendeleza utawala wa kikatiba, utawala bora na wa sheria, kujenga uchumi imara wenye kuleta ushindani na Serikali yangu itajengwa katika misingi iliyowekwa na awamu zilizotangulia, hasa kwa rekodi nzuri ya mtengamano wa uchumi mpana wa nchi na nitafanya marekebisho makubwa katika utumishi wa umma ili uendane na wajibu wake wa kuwatumikia watanzania”, alifafanua Wasira aliongeza kuwa endapo atachaguliwa kuwa Rais, serikali yake itaimarisha kilimo kwa kuleta mapinduzi makubwa ya kilimo na uchumi vijijini na kuondokana na kilimo cha jembe la mkono .
“Jembe la mkono sasa tutalipeleka kwenye jumba la makumbusho, hii itakwenda sanjari na kuwaunganisha wakulima wajiunge katika ushirika ili waweze kukopeshwa matrekta kwa ajili ya kuimarisha kilimo” alisema.
Aidha, alisema endapo atachaguliwa kuiongoza nchi, Serikali yake itaanzisha mjadala wa kitaifa wa kupambana na rushwa, ambapo aliweka bayana kuwa amekuwa ni miongoni mwa viongozi waadilifu waliotumikia nchi bila ya kupata na kashafa yoyote ile “Tutaanzisha mjadala wa kitaifa wa kupambana na rushwa, Baba wa taifa aliwahi kusema anayesema atapambana na rushwa, muangalie machoni kama ana ujasiri wa kupambana na rushwa”, alisema.
“Mimi sina rekodi ya kuwaibia watanzania, mlisikia katika EPA sikutajwa, sakata la Escrow nalo sikutajwa, sio kwamba mimi sifanyi kazi za madaraka, lahasha, Mimi ni Waziri wa Kilimo, ningeweza kuwaibia mbolea, na nimekaa Ikulu muda mrefu, hakuna biashara pale, mkimchagua mla rushwa angalieni atauza hadi Ikulu yenu,” alisema Wassira.
Marais EAC wataka uchaguzi wa Rais Burundi uahirishwe
Marais EAC wataka uchaguzi wa Rais Burundi uahirishwe
WAKUU wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), wameitaka Burundi kuahirisha uchaguzi kwa takribani mwezi mmoja na nusu ili kurejesha hali ya amani nchini humo na kulitaka Bunge kusimamia mchakato huo.
Aidha, wametoa wito wa Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Mataifa (UN)na wadau wengine kuunga mkono juhudi za EAC katika kumaliza matatizo ya Burundi.
Akisoma maazimio ya viongozi hao yaliyofikiwa kwenye kikoa cha pili cha dharura cha kujadili hali ya Burundi kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa EAC, Dk Richard Sezibera alisema maamuzi hayo yanazingatia hali ilivyo nchini Burundi na kutaka kusogeza mbele uchaguzi ili kuweza kurejesha amani nchini humo.
“ Tunazitaka mamlaka zote nchini Burundi kuhakikisha inasitisha uchaguzi kwa muda usiozidi mwezi mmoja na nusu na kuliomba Bunge kusimamia uahirishwaji wa uchaguzi huo,” alisema.
Alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya wakuu hao kupokea taarifa ya mawaziri wa mambo ya nje na wanasheria wakuu au mawaziri wa sheria wa nchini wanachama, ripoti ya mwakilishi wa UN katika Ukanda wa Maziwa Mkuu na ile ya timu ya Wazee wa Jumuia ya Afrika Mashariki inayoongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba..
Uchaguzi wa Wabunge nchini Burundi ulipangwa kufanyika Juni 5 mwaka huu na ule wa rais uliopangwa kufanyika Juni 26. Hii ni mara ya pili kwa EAC kuagiza uchaguzi huo kusogezwa mbele, kwani katika kikoa cha kwanza waliagiza uchaguzi huo kusogezwa mbele kwa muda usiozidi kipindi cha uongozi uliopo madarakani.
Katika kikao cha jana kilichoanza saa 8:20 mchana na kumalizika saa 11:09, ambacho Rais Pierre Nkurunziza aliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Alain Nyamitwe, kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Uganda Yoweri Museveni, huku Rais wa Rwanda Paul Kagame aliwakilishwa na Waziri wa Jumuia ya Afrika Mashariki na Uhusiano Valentine Rugwabiza.
Pia kilihudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, Mwenyeikiti wa Kamishna ya AU, Dk. Nkosazana Dlamini Zuma huku Mwenyekiti wa Ukanda wa Maziwa Makuu, Eduardo Dos Santos aliwakilishwa na katibu wa jumuia hiyo, Profesa Ntumba Luaba.
Sezibera alisema pia EAC imeagiza vikundi vya vijana ambavyo vinaushirika na vyama vya siasa nchini Burundi kunyang’anywa silaha na kuitaka serikali kuweka mazingira mazuri ambayo yatawafanya wakimbizi kurejea nchini mwao.
Aidha, EAC imepongeza kurejea kwa utawala wa kikatiba nchini Burundi baada ya kutokea jaribio la mapinduzi. Akiwa Tanzania kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa kwanza wa EAC waliokutana Mei 13 kujadili mgogoro wa kisiasa nchini humo, majenelali wa juu wa nchi hiyo walifanya jaribio la kumpindua Rais Nkurunziza ambalo lilizimwa na majeshi ya nchi hiyo.
“ EAC inasikitishwa na hali ya nsitofahamu inayoendelea nchini Burundi. Tunawataka wadau kuacha vurugu na machafuko yaliyosababisha vifo, uharibifu wa mali na wengine kukimbia nchi yao.”
Machafuko yalianza nchini humo tangu Aprili 26, mwaka huu na kusababisha zaidi ya vifo 20, huku maelfu wakikimbia nchi yao, yametokana na hatua ya Rais Nkurunziza kutangaza azima ya kuwania muhula wa tatu wa uongozi, jambo ambalo linalalamikiwa na wapinzani kwa madai kuwa ni kinyume na katiba ya nchi hiyo.
MIAKA 16 YA JUMA NATURE YATIA FORA
Nature akiweka maiki vizuri ili akamue ipasavyo.
Mashabiki wakimshangilia Nature baada ya kupanda jukwaani.
.…Akikamua kama kawaida yake.(P.T)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo jana.
(Picha na Freddy Maro / Ikulu)(P.T)
Alhamisi, 21 Mei 2015
Jumapili, 12 Aprili 2015
MLEMAVU MWENYE ULEMAVU MKUBWA KABISA
KWA WALE WENYE MIJI ROHO MIBAYA WASIO NA HURUMA
HAWATAOMBA wala KUSHARE!!!
HAWATAOMBA wala KUSHARE!!!
LAKINI KUMBUKA USIMCHEKE KILEMA!! Na kwa wale wenye Roho ya Huruma NA UPENDO kama mimi Tuombeni pamoja kwa Kuandika "Ameen" Eh Mungu muondole mtoto huyu maumivu!! "AMEEN" na #shareili dua ziwe nyingi kwani dua nyingi zinaumuhimu sana kwa huyu mtoto
Usisahau Kulike Page Hii==>>www.AMRIYNANA.COM
Mwendelezo wa habari ya ajali ya Ruaha Mbuyuni: 6 wadaiwa kupoteza maisha
Mwendelezo wa habari ya ajali ya Ruaha Mbuyuni: 6 wadaiwa kupoteza maisha
- By Admin
- 0 comments
Pichani ni basi hilo baada ya kupata ajali ya kuungua.
Habari zilizotufikia muda huu wa saa nane mchana ni kuwa hadi sasa imeelezwa kuwa watu sita (6) wamepoteza maisha kufuatia ajali ya basi la abiria la Nganga lililogongana na Fuso, na kupelekea magari hayo kuwaka moto, katika eneo la Ruaha Mbuyuni mpakani mwa Morogoro na Iringa.
Hata hivyo, bado kuna ugumu wa habari kamili kutokana na umbali wa eneo hilo la tukio huku tukiharifiwa kuwa, makamanda wa jeshi la Polisi wa Morogoro na Iringa wote simu zao hazipatikani kwa muda mrefu.
Ambapo pia kutokana na ufinyu wa bajeti kwa baadhi ya vyombo vya habari, wameshindwa kufika kwa wakati kwenye eneo la tukio kutokana na kuwa mbali na miji mikuu ya mikoa hiyo ya Iringa na Mbeya.
Kwa mujibu wa ripota wetu kutoka Mkoa wa Morogoro alibainisha kuwa, karibu waandishi wengi wameshindwa kuelekea eneo la tukio kutokana na vyombo vyao kutokuwa na mafuta ya kutosha huku hapo hapo Ofisi za jeshi hilo la Polisi kwa siku ya leo nyingi zikiwa zimefungwa.
MODEWJI BLOG: Hallo!!: Hapo Morogoro tupeni Habari. vipi kuhusiana na ajali ya Ruaha Mbuyuni!.
RIPOTA MOROGORO: “Ni kweli lakini sote tunataka kwenda lakini tumeshindwa huko ni mbali sana.. kutoka hapa Morogoro Mjini hadi hapo ni zaidi ya KM110 ambazo tu unaimaliza mbuga ya Mikumi, ukitoka hapo uanze kuitaafuta Mbuyuni ni zaidi ya KM 35, hivi?.
Unafikiri ni karibu? tumeshindwa hata magari ya abiria tunayoomba lifti, kwa muda huu tutachelewa tu”. Kilieleza chanzo hicho.
Chanzo hicho pia kilibainisha kuwa, kutokana na ajali hiyo kutokea katikati ya mpaka wa Morogoro na Iringa, majeruhi wanaweza kupelekwa Hospitali iliyopo Mikumi ama Iringa mjini.
Modewji blog ilipowasiliana na ripota wa kujitegemea Mkoani Iringa, alibainisha kuwa, hadi sasa bado wanaendelea kukusanya taarifa ila walioweza kupoteza maisha hapo hapo ni sita, akiwemo dereva wa Fuso.
Picha ambazo zimeweza kupatikana ni kwa msaada wa teknolojia ya simu za kisasa zenye uwezo wa kupiga picha na kurusha kwa kutumia intaneti (tehama/ICT) hivyo tunapongeza kwa teknolojia hii na kwa wale walioweza kutuma picha hizi ambazo kwa asilimia kubwa hazikukiuka maadili. ..credit ziende kwa waliopiga hizi picha za ajali, Pia Modewji blog inatoa pole kwa wale wote walioondokewa na wapendwa wao, waliojeruhiwa na kupata matatizo kwenye ajali hiyo.
Modewji blog, tunaendelea kuwasiliana na vyanzo zaidi ilikukupatia habari iliyo bora, endelea kuperuzi nasi.
Jumamosi, 11 Aprili 2015
JANA MJINI MOROGORO LILIFANYIKA LILE TAMASHA LA SANUKA KINOMA NOMA AMBAPO 87.9 ILIMLETA DOGO ASLAY NA OGOPA KOPA,AFANDE SELE,JMOE,TUNDA MANI,MAN DOJO NA DOMO KAYA
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)