Alhamisi, 23 Machi 2017

BURUDANIVIDEOMPYA: Mabibi na Mabwana Young killer ametuletea Remix ya Sinaga Swagga

BURUDANI

VIDEOMPYA: Mabibi na Mabwana Young killer ametuletea Remix ya Sinaga Swagga

Mwimbaji wa bongo fleva Young Killer msodoki ametusogezea video mpya ya wimbo wake wa Sinaga Swagger remix imefanywa na director mtanzania Nicklass, ukimaliza kuitazama naomba uache na comment yako ili Msodoki akipita ajue watu wake wamempokeaje.

Nape Nnauye atumbuliwa, nafasi yake yachukuliwa na Dk. MwakyembeS

Nape Nnauye atumbuliwa, nafasi yake yachukuliwa na Dk. MwakyembeS




Rais Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mheshimiwa Nape Nnauye kama Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Badala yake amemtua Dkt Harrison Mwakyembe kushika nafasi hiyo. Chini ni taarifa ya uteuzi huo mpya:

Jumatatu, 20 Machi 2017

Picha: Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ikiwasili Clouds

Picha: Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ikiwasili Clouds




Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo iliwasili katika ofisi za Clouds Media Group na kuzungumza na uongozi wake kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari waliokuwepo hapo.
Hizi ni baadhi ya picha:

Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akiipokea kamati hiyo

Pichani ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Peter Serukamba ( MB ) akisalimiana na Mkurugenzi wa vipindi na uendeshaji wa kituo hicho, Ruge Mtahaba

AMRIYNANA.COM: Nick wa Pili avipa tano vyombo vya habari, awachana wasanii kuwa ‘makunguru’

AMRIYNANA.COM: Nick wa Pili avipa tano vyombo vya habari, awachana wasanii kuwa ‘makunguru’

Video: Walichosema wabunge na maamuzi ya Waziri Nape kuhusu uvamizi wa Makonda Clouds





Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh. Nape Nnauye, Jumatatu hii, March 20, alikwenda katika makao makuu ya Clouds Media Group kufuatia taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenda kwenye kituo hicho akiwa na askari wenye silaha na kuwataka watangazaji wa kipindi cha Da W’keend Chat Show kurusha kile alichokiita kipindi chake.



Waziri Nape ameunda tume ya uchunguzi ya watu watano watakaongozwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo, Hassan Abbas, na kutoa masaa 24 kwa tume hiyo kuzungumza na Mkuu wa Mkoa Makonda na kutoa ripoti yake Jumanne hii, March 21, 2017.

Nick wa Pili avipa tano vyombo vya habari, awachana wasanii kuwa ‘makunguru’

Nick wa Pili avipa tano vyombo vya habari, awachana wasanii kuwa ‘makunguru’






Rapper Nick wa Pili amefurahishwa na umoja uliooneshwa na vyombo vya habari katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na hali tete baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia kituo hicho Usiku wa Ijumaa iliyopita kutokana na video za CCTV kamera zilivyoonyesha.
Nick ametoa pongezi hizo kupitia mtandoa wa Twitter lakini pia amewachana wasanii wenzake ambao wamekuwa hawana umoja katika kutafuta maslahi yao.